📍 Makao Makuu: Dar es Salaam, Tanzania
🕰 Imeanzishwa: 2022
👤 Mkurugenzi Mtendaji: Ally Zayumba
Mafia Boxing Promotion ni taasisi ya kisasa yenye makao yake Dar es Salaam, inayojikita katika kukuza na kuendeleza vipaji vya mchezo wa ngumi hapa Tanzania. Kupitia mafunzo ya kitaalamu na mapambano ya kulipwa, taasisi hii imekuwa chachu ya mafanikio kwa mabondia chipukizi na wataalamu. Ikiongozwa na Ally Zayumba (CEO), Mafia Boxing Promotion ina timu imara inayoongozwa na Khamisi Mwakinyo (Kocha Mkuu), Anatol (Meneja wa Matukio), na Manager Tozzi (Afisa Ustawi wa Mabondia). Kwa pamoja, wanahakikisha mabondia wanapata maandalizi bora, nidhamu ya hali ya juu, na fursa za kimataifa.
Mafia Boxing Promotion ni kampuni iliyojikita kwenye mchezo masumbwi, na kwa sasa inasimamia takriban mabondia 20 ambao tayari wamefanikiwa kutwaa mataji ya ubingwa wa dunia. Kampuni hii ilianzishwa miaka mitatu iliyopita, na tangu wakati huo imepiga hatua kubwa na inaendelea kupata mafanikio makubwa katika tasnia ya masumbwi.
Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada wake endelevu, ambao umechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wetu. Msaada na hamasa yake vimetuwezesha kulea vipaji, kupanua wigo wetu, na kuinua mchezo wa masumbwi ndani ya nchi na kimataifa.